Lengo Letu

Naturalliance ni ya kuwaongoza watu kurejesha na kuendeleza mali na huduma za mazingira wanakoishi.

 

Mfumo wa Ikolojia wa ulimwengu na raslimali yake.

Muinuko wa dunia ulivyoonekeana Kutoka kwa Apollo 8 katika mzunguko wa mwezi © NASA
Muinuko wa dunia ulivyoonekeana Kutoka kwa Apollo 8 katika mzunguko wa mwezi © NASA

Fikiria ulimwengu kama mpira wa miguu ulioshikwa kati ya mikono yako iliyonyoshwa. Hewani, au sehemu inayosaidia maisha juu na chini ya ardhi au majini, ni ndogo kuliko unene wa ukucha wa kidole! Hewa hiyo inayoweza kuharibiwa kwa urahisi ina michoro maridadi ya mitindo, iliyo na mimea, wanyama na viumbe vingine, na ardhi, maji na hewa inayovisidia. sisi ni mojawapo ya mfumo huu wa ikolojia ikiwemo misitu, milima, nyasi, jangwa, maziwa, mito na bahari. Tunatehemea afya na rasilimali ya ikolojia ya ardhi kujikimu.

Viumbe ndani ya mfumo wa ikolojia

Aina ya ndege wa kijivu anayeitwa Partrige, chanzo muhimu cha afya ya ardhi ya ukulima  © Matej Vranič
Aina ya ndege wa kijivu anayeitwa Partrige, chanzo muhimu cha afya ya ardhi ya ukulima © Matej Vranič

Sasa fikiri idadi ndogo ya viumbe (mimea, wanyama, kuvu au viumbe vingine vidogo) katika mfumo wa ikolojia ulio na chakula kingi na makao, na uchache au ukosefu wa wanyama wanaokula wanyama wengine, magonjwa, wadudu, au njia nyingine za vifo. Majaribio yanaonyesha kwamba idadi kama hii itaongezeka. Wakati wa kuongezeka unatofautiana na ukubwa wa viumbe, bakteria zikiongezeka mara mbili kwa dakika chache lakini itachukua miaka kumi au zaidi kwa ndovu, ilhali idadi ya wanyama wadogo na mimea ikiweza kuongezeka mara kadhaa kwa mwaka. Idadi kama hizi mwishowe hufikia kikomo katika kutumia raslimali na huangamia kwa sababu ya njaa. Wakati mwingi hata hivyo, idadi ya mimea iliyokomaa na wanyama haiongezeki hivi. Ajali, ulaji wanyama wengine, na magonjwa huchukua idadi kubwa ya changa iliyoko kwa sababu ya kuongeza idadi, huku chache zikifa njaa. Chache bado hufika 'uzeeni'. Vifo hutoa nafasi ya viumbe vingine katika mfumo wa ikolojia kustawi, ikiwemo sisi.

Athari zetu kwa mfumo wa ikolojia.

Binadamu waliishi kama wawindaji na watafuta chakula mwituni kwa milenia nyingi kabla ya kujifunza kufuga wanyama na kupnda mimea. Kilimo kilivuma baada ya wakati wa mwisho barafu kali, ikileta njia imara ya usambasaji wa chakula ulioruhusu maisha ya binadamu kustawi na kunawiri, kupelekea kuchipuka kwa majiji. Idadi ya binadamu imeongezeka sana, ikileta uharibifu mkubwa kwa mfumop wa ikolojia na hali ya hewa. Iwaapo itakatizwa zaidi ya kiwango fulani cha dharura, mifumo ya ikolojia itasita kuendeleavizuri, mwishowe kuleta athari za shida kwa hali ya maisha ya binadamu vile vile hali nyingine za mazingira. Mashambani, shughuli zetu zinaweza kuleta uvunaji zaidi wa viumbe mwitu mifumo isipothibitiwa vizuri. Majijini tunategemea ukulima wa mifumo ya ikolojia kwingineko kwa uzalishaji mkubwa wa raslimali. Katika ulimwengu wa kisasa, ni wanachi wache sana wanaelewa mchakato husika, na sheria zinazowekwa na wengi wa walio mijini wakati mwingi huwa hazijulikani na jamii mashambani. Idadi ya binadamu ikiwa juu sana kuliko ilivyotarajiwa, ni vigumu sana kuzuia athari zinazileta uharibifu kwa kiwango cha mfumo wa ikolojia bila ya uamuzi wa pamoja na ulio sahihi, kutumia sayansi na ujuzi wa vitendo.