Kusuluhisha shida

Siasa ndogo ndogo ni heri kijumla kuliko siasa kali, kama tu vile raslimali mwitu hunufaika kutoka kwa mabadiliko ya polepole katika mipaka ya makao © Lauri Kovanen
Siasa ndogo ndogo ni heri kijumla kuliko siasa kali, kama tu vile raslimali mwitu hunufaika kutoka kwa mabadiliko ya polepole katika mipaka ya makao © Lauri Kovanen

Ujuzi unaweza kufunza watu kuwa demokrasia ni njia nzuri zaidi ya uongozi kuliko uongozi wa mtu mmoja, halafu kuepuka wanasiasa wanaokuza mgogoro au ni wachoyo kiuchumi au wasioweza kufanya kazi; hivyo pia watu wanahitaji kujifunza kuhusu njia nzuri zaidi za kuhifadhi utajiri wa mazingira. Kama vile kwa shughuli zote za kibinadamu, usawa na uvumilivu unaweza kufanya kazi vizuri kuliko misimamo mikali. Huku sehemu kubwa ya ardhi ikisimamiwa kwa kiwango fulani na binadamu, utajiri wa mazingira unaweza kuwepo vyema zaidi iwapo manufaa yake yanathaminiwa sana, si kwa kula mimea tu na kutazama filamu za kimazingira lakini pia kwa kufurahia uwepo wa wanyama wengine na, ikiwezekana kwa vitendo, kutafuta chakula kama wao pia. Pia ni busara kwa watu kuelewa jinsi inavyoweza kuwa vigumu, kijamii na kiekolojia, kuthibiti utajiri wa mazingira wakati huo huo tukipanda mimea. Kuelewa umuhimu wa uthibiti huu mara mbili unahitaji kuenea kwa jamii kila pahali.

Viumbe visivyokaribishwa

Wawindaji wa Ulaya wanaweza kupanga kuisaidia serikali.
Wawindaji wa Ulaya wanaweza kupanga kuisaidia serikali.

viumbe wakati mwingine huwekwa kwa makusudi au kiajali, katika sehemu ambazo havikusimamia kiasili. Ni vigumu kuvithibiti viumbe vigeni hivi iwapo vitaenea kwa haraka na bila kugunduliwa. (k.m viumbe vilivyozaliwa majini, ikiwemo mimea). Kama vitadhuru mfumo wa ikolojia,lazima viondolewe. Utaalamu mkubwa wa shughuli hii umeendelezwa katika Oceania. Wenyeji, haswa wawindaji na wavuvi, wanaweza kuchangia wakati wa kuangalia, na mpangilio pahali ambapo wako na hii ni ya thamani katika kampeni za uondoaji. Kwa kampeni kama hizi kufaulu kijamii, umma wanahitaji kuona manufaa mara moja na kujua kwamba viumbe vilivyowekwa vinatolewa kwa njia ya kibinaadamu.

Kudhibiti wanyama wanaokula wengine na wadudu.

Wakati mwingine ni vigumu kutokuwa na panya kwenye maduka ya vyakula  © Torook/Shutterstock
Wakati mwingine ni vigumu kutokuwa na panya kwenye maduka ya vyakula © Torook/Shutterstock

Vizuizi vivyo hivyo vya kijamii hutumika kwa udhibiti wa wanyama wanaokula wanyama wengine na wadudu. Udhibiti huhitajika wakati mwingine kuhifadhi maisha ya binaadamu na mali, na hali ya kimaisha katika mfumo wa ikolojia ambapo binaadamu wanashindana na viumbe vingine kula mazao au kutumia wanyamapori kujitunza. Baadhi ya jamii kote ulimwenguni zinaendeleza njia za kitamaduni kusimamia utajiri wa mazingira, kupitia kukubali kwa viumbe vinavyoleta shida na kuhusisha njia za kitamaduni zinazoziruhusu viumbe hivi kuendelea kuwepo. Kwingineko, kubadilishwa kunaweza kuelekeza mfumo wa ikolojia zaidi kwa kupendelea wanyama wanaokula wanyama wengine kijumla, hivyo basi kusababisha hatari ya uwezekano wa kutoweka kwa mawindo yasiyopatikana kwa urahisi kama vile ndege wanaotaga ardhini ulaji wanyama usipoangaliwa. Hata sehemu ambazo viumbe hawavumiliwi, udhibiti unaopendelewa utakuwa, kwa sababu za kibinaadamu na uchumi, kutenga na kuzuia wanyama wanaokula wanyama wengine na wadudu. Njia nyingine, ya kupunguza idadi ya wanyama wanaokula wanyama wengine na wadudu, mara nyingi huwa na pingamizi kutoka kwa wale wanaopeana kipaumbele kulinda wanyama binafsi. Katika hali hii, ni muhimu sana kwa uthibiti wowote kutilia maanani sayansi thabiti na ulinzi mwingine kuruhusiwa, kwa mfano kuwa na maeneo kuhifadhi idadi ya viumbe husika ambapo havisababishi shida. Uondoaji kabisa wa viumbe (isipokuwa vinavyosababisha magonjwa) haukubaliki kwa jumla katika jamii za kisasa. Hata hivyo, utawala asili mara nyingine au kuweka kimaksudi tena husababisha haja ya kudhibiti idadi tena.

Suluhisho kulingana na mazingira.

Uboreshaji wa mitandao kwa viumbehai misitu na uthibiti wa mafuriko kwa ongezeko la makazi © IUCN
Uboreshaji wa mitandao kwa viumbehai misitu na uthibiti wa mafuriko kwa ongezeko la makazi © IUCN

Suluhisho kulingana na mazingira ni ni njia ya kuhifadhi, kuthibiti kujisimamia na kerejeshamifumo ya ikolojia asili na iliyorekebishwa kwa njia zinazotoa ustawi wa binadamu na manufaa kwa viumbehai. Kwa mfano, gharama ya kurejesha afya ya mfumo wa ikolojia wa ardhi nyevu inaweza kuwa chini kuliko kulipa ili kusafisha maji kutoka kwa mifumo iliyoharibiwa, haswa manufaa kama thamani ya burudani ya mifumo iliyorejeshwa inapozingatiwa. Suluhisho zonaweza kutofautiana kwa ukubwa kutoka kwa kubwa zaidi na ya muda mrefu, kama vile majukumu ya upandaji mititena ili kurejesha hewa ya kaboni na kupunguza mafuriko, hadi ndogo zaidi na ya muda mfupi, kama vile kupandia wadudu wanaokula wadudu mimea sehemu ndogo ya mimea karibu na mimea mawindo ya wadudu hao ambayo wangukula.